Pages

Saturday, June 23, 2012

Sababu za wakristo kuabudu Jumapili

Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-

a) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].

b) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].

c) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]

d) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].

e) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.

Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].

KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA

Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].

Anin Gift

Saturday, June 9, 2012

Waimbaji ”KWETU PAZURI” Wawasili Dar Leo

 

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka jijini Kigali nchini Rwanda imewasili leo Jijini Dar es salaam wakitokea nchini kwao Rwanda, tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji katika mkutano mkubwa wa kimataifa unaofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kundi la kwanza la kwaya hiyo liliondoka jana kwa njia ya basi kuja jijini, huku kundi la pili ndio limewasili leo mchana.

Hii itakuwa mara ya nne kwa waimbaji hao kufika nchini ambako wamekuwa na mashabiki lukuki, kutokana na uimbaji wao, ambapo safari hii wanatarajia kuwepo kwa wiki nzima jijini Dar es salaam ikiwa maalumu kwa mkutano huo,Pia wanatarajia kuwasili na toleo lao jipya la kanda ambalo baadhi ya nyimbo zimeanza kusikika katika vituo vya radio za injili jijini Dar es salaam.