Pages

Friday, February 22, 2013

NIDHAMU NI NINI?

Nidhamu ni uwezo wa kufanya mambo / vitu fulani pasipo kufuata hisia (kinyume na ulivyozoea). Baada ya kutoa tafsiri hiyo fupi iliyobeba shehena ya maarifa na uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu binafsi, James alizungumzia na kufafanua maeneo nane (8) ambayo yanahitaji nadhamu kali.


UNATAKIWA UWE NA NIDHAMU KALI KATIKA MAENEO NANE (8).

1. Eneo la kujiwekea malengo binafsi kila mwaka.

* Kujiwekea fursa/possibilities; mfano. mwaka huu nitafanya a, b, c... ukiendelea zaidi utatoka kwenye mwaka itakuwa malengo ya mwezi hatimaye kila siku.
* Mtu mwenye malengo anajua kule anakoenda, mtu asiye na malengo hawezi kwenda na hajui anakokwenda.
* Malengo yanakupa uwezo wa kudhibiti mabadiliko ya maisha katika dunia.
* Malengo yatakupa FOCUS.
* Siri moja ya mafanikio duniani ni kuwa na FOCUS.
* Malengo yatakufanya uwe namba moja (1), Mafanikio yanakuja kwa kufanya yale uliyojiwekea kuyafanya.


2. Nidhamu ya kufikiri vizuri / clear thinking.

* Ni uwezo wa kufikiri vizuri bila bughudha.
Hapa ananukuu msemo mmoja usemao; Those who cannot go within cannot go without.
* Mali ni uwezo wa mtu kufikiri vizuri / uwezo wa kutumia akili vizuri/zaidi.
Nukuu chanya: 'TATIZO SIO UDONGO TULIO NAO BALI UBONGO TULIO NAO'
* Njia rahisi ya kufikiria vizuri ni kuuzoeza ubongo kufikiri.

3. Nidhamu ya kutunza muda / time management.

- Tatizo tulilo nalo ni kutokutunza muda.
* Maisha ya mtu yeyote yanawakilishwa na kitu kidogo kinachoitwa muda, ukipoteza muda unapoteza maisha yako.
* Kimsingi maisha yako ni muda wako, na muda wako ni maisha yako. Jaribu kujitathmini je! kila baada ya dakika 15 umefanya nini. Usijipe mwanya, usikubali kuchelewa.

4. Nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii / deligent / hard working.

* Hakuna sehemu nzuri ya kufanikiwa kama Tanzania kwa sababu watu wengi ni wavivu, watu wengi sio wabunifu (wana-copy na ku-paste).
* Ukifanya kazi kwa masaa ya kawaida utakuwa na maisha ya kawaida, ukifanya kazi kwa masaa yasiyo ya kawaida utakuwa na maisha ya juu zaidi / yasiyo ya kawaida.
* Kama unapenda starehe, fanya kazi kwa nguvu zaidi kuliko mtu yeyote yule.

5. Nidhamu ya kujitunza kiafya.

6. Nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza.

* Kama huwezi kujiwekea akiba mara kwa mara basi uwezo wa ukubwa haupo ndani yako.
* Kuwekeza ni suala la kuwa na miradi.
* Kuwekeza ni kutumia baadhi ya vitu / kitu ulicho nacho kutengeneza mkondo mwingine wa fedha.
* Ukitaka kuwa maskini tumia fedha zote ulizo nazo na ziada kidogo, fedha ambayo huipangilii itaondoka.


7. Nidhamu ya ujasiri / ushujaa / courage.

* Kila mtu duniani anaogopa kitu fulani, Lakini watu ambao wanapanda juu ni wale wanaoishinda hofu / woga. Kuna hofu ya kweli na isiyo ya kweli.
* Jaribu kuzishinda hofu zako, usipozishinda maisha yako yatabaki pale pale.
* Ujasiri unakufanya uwe na uwezo wa kumiliki mambo makubwa / biashara kubwa.

8. Nidhamu ya kujifunza endelevu / continuous learning.

* Kama kuna udhaifu Tanzania ni udhaifu wa kutopenda kujifunza.
* Mtu yeyote ambaye hana tabia ya kusoma ni sawa na mtu ambaye hajui kusoma.
* Nidhamu ya kujifunza ni Elimu binafsi.

Tuesday, January 1, 2013

MAMBO 7 YATAKAYO KUSAIDIA KUTIMIZA NDOTO YAKO




  1. Katika ndoto ulizo nazo, chagua NDOTO moja uanze nayo(ukimbie nayo)
  2. Amini NDOTO yako, uliyonayo siku moja itakuwa kwenye uhalisia
  3. Omba msaada kwa waliokutangulia, mfano NDOTO yako ni kuandika vitabu kuna watu walishaandika vitabu kabla yako,
  4. Kuna nyakati unabidi ubadili mfumo wa maisha yako, ili kuweza kufikia NDOTO yako.
  5. Weka kikomo cha kufanya NDOTO yako, mfano, unataka kuandika kitabu unaweka kuwa utaandika kwa mda gani, labda utaandika kwa miezi 18.
  6. Waambie watu wengine kuhusiana na NDOTO yako uliyonayo, kwasababu unapo tamka neno, kunanguvu, kumbuka hilo, 
  7.  Karika kila Safari kuna vikwazo, usiogope kwa vikwazo vitakavyotokea, na chuga visiwe chanzo cha kutaka kuua NDOTO YAKO

Saturday, June 23, 2012

Sababu za wakristo kuabudu Jumapili

Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-

a) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].

b) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].

c) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]

d) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].

e) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.

Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].

KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA

Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].

Anin Gift

Saturday, June 9, 2012

Waimbaji ”KWETU PAZURI” Wawasili Dar Leo

 

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka jijini Kigali nchini Rwanda imewasili leo Jijini Dar es salaam wakitokea nchini kwao Rwanda, tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji katika mkutano mkubwa wa kimataifa unaofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kundi la kwanza la kwaya hiyo liliondoka jana kwa njia ya basi kuja jijini, huku kundi la pili ndio limewasili leo mchana.

Hii itakuwa mara ya nne kwa waimbaji hao kufika nchini ambako wamekuwa na mashabiki lukuki, kutokana na uimbaji wao, ambapo safari hii wanatarajia kuwepo kwa wiki nzima jijini Dar es salaam ikiwa maalumu kwa mkutano huo,Pia wanatarajia kuwasili na toleo lao jipya la kanda ambalo baadhi ya nyimbo zimeanza kusikika katika vituo vya radio za injili jijini Dar es salaam.